Facebook yapigwa faini zaidi ya dola za Kimarekani milioni miamoja na ishirini  - kira siku

Breaking

RECENT POST

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 19 May 2017

Facebook yapigwa faini zaidi ya dola za Kimarekani milioni miamoja na ishirini 



Tume ya Ulaya imeupiga faini mtandao wa kijamii Facebook ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni miamoja na ishirini kwa kutambua kwamba walikuwa wakiwapa maofisa wa umoja wa Ulaya taarifa potofu wakati walipokuwa wakinunua app ya ujumbe mfupi wa maneno wa WhatsApp mnamo mwaka 2014.

Tume hiyo imesema kwamba wakati wa makubaliano hayo tathimini iliyofanywa ilithibitisha kuwa hakutakuwa na muunganiko baina ya mtandao wa kijamii wa Facebook na akaunti za WhatsApp , hata hivyo mtandao huo uliendelea kuwapa wateja uchaguzi wa nini cha kufanya na hivyo kutokuwa na kizuizi.

Kamishna wa tume hiyo ya Ulaya, Margarethe Vestager, amesema kuwa hatua hiyo dalili kwamba kampuni zinapaswa kutoa taarifa sahihi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages